ARSENAL 4-0 NOTTINGHAM FOREST, CHELSEA, LIVER ZASHINDA

0 comments
Nicklas BendtnerLucas Perez alifungia klabu ya Arsenal mabao yake ya kwanza na kuwasaidia Gunnerskupata ushindi mkubwa dhidi ya Nottingham Forest na kufika raundi ya nne Kombe la Ligi Uingereza (EFL).
Granit Xhaka aliwaweka Arsenal kifua mbele kwa kombora la hatua 30 kutoka kwenye goli dakika ya 23.
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicklas Bendtner alishindwa kufunga penalti upande wa Forest kabla ya Lucas kuongeza ushindi wa Arsenal kupitia mkwaju wa penalti baada ya Chuba Akpom kuchezewa visivyo dakika ya 60.
Lucas kisha alimbwaga kipa na kufunga bao lake la pili usiku huo dakika ya 71 kabla ya Alex Oxlade-Chamberlain kukamilisha ushindi wao dakika ya 93.
Ilikuwa mara ya pili kwa Lucas Perez kuanza mechi Arsenal tangu ajiunge nao kutoka Deportivo La Coruna mwezi Agosti.
              
Nicklas Bendtner alijiunga na Nottingham Forest 7 Septemba kutoka Wolfsburg ya Ujerumani.

MECHI NYINGINE ZA JUMANNE 20 SEPTEMBA 2016
  • Bournemouth 2-3 Preston
  • Brighton 1-2 Reading
  • Derby 0-3 Liverpool
  • Everton 0-2 Norwich
  • Leeds 1-0 Blackburn
  • Leicester 2-4 Chelsea
  • Newcastle 2-0 Wolves
  • Nottm Forest 0-4 Arsenal


Read More »

MAREKANI YAISHUTUMU URUSI SHAMBULIZI LA SYRIA

0 comments
Marekani imesema ndege za kivita za Urusi zilihusika kushambulia msafara wa misaada nchini Syria siku ya Jumatatu na kusababisha vifo.
Maafisa wa Marekani wameiambia BBC ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, zilikuwa angani, sambamba na msafara huo wa magari, wakati tukio hilo likitokea.
Hata hivyo Urusi imekana na kusema kuwa ndege hizo hazikuwa zake wala za Syria, na kutupia lawama wapiganaji wa waasi.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege zake zinazojiendesha zenyewe zilikuwa zikifuatilia msafara huo, lakini kamera zao zilijizima kabla ya mashambulizi kuanza.
Shambulio hilo la Jumatatu lilifanyika saa kadhaa baada ya serikali ya Syria kutangaza kumaliza wiki ya kusitisha mapigano.

CHANZO:BBCSWAHILI.COM

Read More »

RYAN GIGGS ATEULIWA KOCHA/MCHEZAJI MANCHESTER UNITED

0 comments
MANCHESTER CITY-UINGEREZA,Klabu ya Manchester United leo imemtangaza mchezaji mkongwe zaidi wa klabu hiyo kuwa kocha wakati akiwa bado anaendelea kuichezea klabu hiyo.

Taarifa hizo zimethibitishwa na mtandao rasmi wa Manchester United kwamba Giggs ambaye hivi karibuni alimaliza mafunzo yake ya ukocha atakuwa mmoja ya jopo la makocha watakaomsaidia David Moyes kuendesha jahazi liloachwa na Sir Alex Ferguson.

Pia wakati huo huo kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba David Moyes amemteua Phil Neville kuwa kocha wa timu ya kwanza.

Read More »

JESHI NCHINI MISRI LAMPINDUA RAIS MOHAMED MORSI.

0 comments
The Egyptian army has toppled President Mohammed Morsi. (Amr Nabil/Hassan Ammar/AP) 
 
us-egypt-morsi.jpeg2-1280x960 
Jeshi nchini Misri limemuondoa madarakani Rais aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini humo Mohamed Morsi na imemteuwa kiongozi wa muda wa nchi baada ya maandamano makubwa yanayoipinga serikali.

Akihutubia kwa njia ya televisheni jumatano jioni, mkuu wa jeshi, Abdul Fatah Khalil Al-Sisi alisema katiba ya Misri imesitishwa kwa muda na mkuu wa mahakama ya katiba ameteuliwa kuwa kiongozi wa muda nchini humo. Sisi alitangaza kwamba jeshi linaangalia watu wa Misri kufuatana na maandamano makubwa ya upinzani yakidai kuwa Rais Mohamed Morsi ajiuzulu.

Kufuatia hotuba ya kwenye televisheni Bwana Morsi alitoa taarifa kupitia akaunti yake ya Twitter, akiita hatua ya jeshi ni “mapinduzi kamili”. Aliwasihi wa-misri wote kukataa hatua ya jeshi lakini pia aliwataka kuwa na amani.

Kiongozi mpya wa muda nchini Misri, Adli Mansour ana umri wa miaka 68 ni mkuu wa sheria katika mahakama ya juu ya katiba. Ataapishwa alhamisi.Kusoma zaidi bofya

Kama sehemu ya mwongozo mpya unaoungwa mkono na jeshi kwa nchi, sisi aliutaka uchaguzi wa urais na wabunge, jopo kutathmini katiba na kamati ya mashauriano kitaifa. Alisema mwongozo ulikubaliwa na makundi kadhaa ya kisiasa. 

Pia aliwasihi watu wa Misri kuepukana na ghasia. Jeshi lilimpa Bwana Morsi saa 48 kutatua matatizo ya kisiasa au kuwepo hatari ya jeshi kuingilia kati. Viongozi wa jeshi walisema wataweka “mwongozo” kama tofauti kati ya serikali ya ki-islam na wapinzani wake hawatamaliza matatizo yao ifikapo jumatano mchana ya tarehe tatu mwezi wa saba mwaka 2013. Tarehe hiyo ya mwisho ilipita muda wake bila ya hatua zozote kuonekana. 

Bwana Morsi hakika alikataa wito wa kujiuzulu na aliapa kuendelea kubaki madarakani hata kama itamsababishia kifo chake. Pia alilalamika jeshi kutoa kitisho chake cha kuingilia kati katika matatizo ya kisiasa. 

Baruti zilipaa angani kwenye umati wa watu wanaocheza na kupeperusha bendera katika uwanja wa tahriri Square mjini cairo, kiini cha ghasia za mwaka 2011 ambazo zilimuondoa Rais wa muda mrefu nchini Misri, Hosni Mubarak.

Katika wiki ilizopita maandamano yenye ghasia kati ya wafuasi na wapinzani wa bwana Morsi yameuwa takribani watu 40. Jeshi la Misri limetangaza kuchukua madaraka ya nchi hiyo huku likitangaza kuwa si mapinduzi lakini Mohamed Morsi si rais tena wa Misri. Tayari Saudia Arabia imetuma salamu za pongezi kwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo kwa kluchukua madaraka.

Hali ya rais Morsi ilikuwa ngumu pale wananchi wake walipoamua kuingia mitaani kumpinga siku chche zilizopita kwa maandamano baada ya kujitwalia madaraka mengi kiutawala kama mtangulizi wake.(Chanzo: BBC)

Read More »

Rais Obama awasili, aisifu Tanzania

0 comments



Dar es Salaam. Rais Barack wa Marekani, Obama ametaja vipaumbele vinne vya Marekani kwa Tanzania, ambavyo vinajumuisha miradi mbalimbali ya umeme, miundombinu ya barabara, maji na programu za vijana kwa lengo la kuongeza ajira.
Kiongozi huyo aliwasili Dar es Salaam jana mchana ikiwa ni nchi ya mwisho katika ziara yake barani Afrika ikitanguliwa na Senegal na Afrika Kusini.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Rais Obama alisema aliainisha mambo hayo wakati alipozungumza na mwenyeji wake huyo.
Alisema katika mazungumzo hayo, waligusia mradi wa mkubwa wa umeme uitwao Power Afrika wenye lengo la kuongeza kiwango cha umeme kinachozalishwa nchini na barani Afrika ili kupata umeme nafuu na wa uhakika utakaochagiza kuongeza uzalishaji na kukuza ajira.
Nchi nyingine za Afrika ambazo zitanufaika na mpango huo ni Kenya, Ghana, Liberia, Nigeria na Ethiopia.
Rais Obama alisema pia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo, ukuzaji wa demokrasia na utawala bora. Alimzungumzia pia mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hashimu Thabeet anayecheza katika Ligi Kuu ya Marekani (NBA), akiwa na timu ya Oklahoma Thunder ya Marekani, akisema hawakuzungumzia suala lake na kuahidi kufanya hivyo siku nyingine.
Akijibu swali iwapo anaridhishwa na misaada ambayo nchi yake inatoa kwa Tanzania, Rais Obama alisema anafarijika kwa matunda yanayopatikana katika mapambano dhidi ya malaria, barabara mpya zinazojengwa na katika maeneo mbalimbali ya nchi.
“Hatutoi dawa, bali tunajenga miundombinu ya afya, hatutoi chakula, bali kuwezesha nchi kujitosheleza kwa chakula pia tunasisitiza kubadilishwa kwa sheria mbalimbali ili kutoa fursa kwa sekta binafsi kuleta mitaji yao kwa wingi zaidi, lakini jambo la muhimu ni kuijenga Afrika,” alisema.
Kuhusu sekta ya utalii, Rais Obama alisema watatangaza vivutio vya Tanzania, lakini kwa kuwa ameambiwa ujangili ni tatizo, Serikali yake itaisaidia Tanzania kukabiliana na changamoto hiyo.
“Tutatangaza utalii, nimeelezwa ujangili ni tatizo hivyo Marekani itasaidia kupambana na changamoto hiyo na tutaongeza fedha kuhakikisha hali hiyo inatokomea,” alisema.
Akichangia hoja ya misaada ya Marekani, Rais Kikwete alisema Mradi wa Maendeleo ya Changamoto za Milenia (MCC), umekuwa msaada mkubwa kwa Tanzania.
Alisema kupitia MCC, Tanzania imepata msaada wa kujengewa barabara katika maeneo ya vijijini na yale yanayozalisha chakula kwa wingi.(MWANANCHI)

Read More »

OBAMA KUTUA LEO TANZANIA-ATAINGIA SAA NANE MCHANA

0 comments
Rais wa Marekani, Barack Obama anatua nchini kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni hatua yake ya mwisho ya ziara yake barani Afrika.
Dar es Salaam. Yametimia! Baada ya siku kadhaa za kusubiri kwa hamu, vitabu vya historia ya Tanzania vinaongezewa kumbukumbu wakati Rais wa Marekani, Barack Obama atakapowasili nchini leo mchana kwa ziara ya siku mbili. Ndege ya Air Force One itakayombeba  Obama na msafara wake itakanyaga ardhi ya Tanzania saa 8.40 mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambako atapokelewa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
 Obama ambaye anafuatana na mkewe Michelle na binti zake, Malia na Sasha, anatua Tanzania ikiwa ni sehemu yake ya mwisho ya ziara yake barani Afrika.
Anawasili Tanzania akitokea Afrika Kusini ambako alikwenda Ijumaa baada ya ziara yake ya Senegal.
Historia imetimia
Imepita miaka 50, tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alipotembelea Marekani, Julai 13, 1963 na kukutana rais wa nchi hiyo wakati huo, John F Kennedy na ziara hiyo inaaminika kuanzisha urafiki wa viongozi hao ambao umedumu hadi sasa. 
Ujio wa Rais Obama una maana na faida kubwa kwa Tanzania katika maeneo ukiangalia kihistoria, kisiasa, kidiplomasia na kiuchumi pia.
Ziara ya  Obama ni heshima kubwa kwa Tanzania na itaingia katika vitabu vya kihistoria kwani ana rekodi ya kuwa mtu mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuongoza taifa la Marekani. Kuchaguliwa kwake (Obama), ambaye baba yake mzazi alikuwa na asili ya Kenya kuliashiria nuru mpya kwa siasa za Marekani kwani watu weusi wa taifa hilo kwa miaka mingi walikuwa wakipigania haki za kufaidika na fursa za kiuchumi na kisiasa katika taifa la Marekani.
Tanzania, kwa miaka mingi ilikuwa inaunga mkono harakati za watu weusi na ndiyo maana iliikuwa karibu na viongozi wa harakati za kupigania haki za watu weusi.
Mwalimu Julius Nyerere alikuwa karibu na Martin Luther King na mkewe Correta , ambao waliongoza harakati za mtu mweusi kujikomboa.Pia, viongozi wengine wa harakati hizo za mtu mweusi kutambuliwa kule Marekani, Jesse Jackson, Andrew Young na Malcolm X waliitembelea Tanzania mara nyingi.    Obama alipochaguliwa kushika nafasi hiyo mwaka 2008 alifurahiwa na wapenda amani kote duniani na hasa Waafrika kwani walimhesabu kuwa ni sehemu yao.
Kuja kwake leo ni heshima kubwa kwani Tanzania inakuwa nchi ya nne  Afrika kutembelewa na Obama baada ya Ghana mwaka 2009 na ziara yake ya hivi karibuni ya nchi za Senegal na Afrika Kusini.
Ukizingatia kuwa  Obama  ana miaka mitatu na nusu kabla ya kumaliza kipindi chake cha pili cha uongozi wake huenda ziara hii ndiyo ikawa ya mwisho kwake barani Afrika akiwa na wadhifa wa rais.

Read More »
0 comments
"Ziara ya Rais Xi kwa Tanzania imeonesha kuwa China haina malengo ya muda mfupi na Afrika, bali ya muda mrefu pamoja na kujenga urafiki wa karibu.". "
- Frans-Paul van der Putten, Mkuu wa kitengo cha utafiti chuo cha Uhusiano wa kimataifa Uholanzi

Read More »