PAPA ASTAAFU RASMI

http://www.bbc.co.uk/news/special/panels/13/feb/pope_resigns/img/pope_resigns976x511v2.jpg 

VATICAN-ITALIA,
"Ahsante na usiku mwema" Hayo ndiyo maneno ya mwisho ya kiongozi na mchungaji wa waumini zaidi ya bilioni 1.2 wa Kikatoliki dunia nzima Papa Benedict XVI, alipokuwa akijiuzuru rasmi hapo jana saa 8:00 usiku saa za Italia(Sawa na saa 4:00 usiku Afrika mashariki)

Huo ndiyo ulikuwa wakati ambao papa huyo amemaliza kipindi chake rasmi na kubaki kumbukumbu akivaa cheo kipya cha papa mstaafu, akiweka rekodi ya kuwa papa wa miaka ya hivi karibuni kujiuzuru.

Akiwahutubia maelfu ya watu katika uwanja wa St.Peter's Papa amesema amejiuzuru siyo kwa faida yake bali kwa faida ya kanisa.
akiongeza " Mimi siyo papa tena lakini bado nipo ndani ya kanisa, naanza safari yangu ya mwisho kama mtalii ndani ya dunia hii"

Baada ya kujiuzuru papa huyo arirudi na helkopta iliyomleta kwenda Castle Gandolfo ambako ndiko makao yake mapya kama papa mstaafu ndai ya Vatican.

Kujiuzuru huko kunafungua mlango mpya kwa mchakato wa uchaguzi wa papa mpya ambapo bado haijafahamika ni nani atakuwa mrithi wa papa huyo.

0 comments: