MPANGO WA KUMPINDUA RAIS KABILA

LIMPOPO-AFRIKA KUSINI, Raia kumi na tisa wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo wanaoshukiwa kuwa waasi wamefunguliwa mashtaka nchini Afrika Kusini kwa njama ya kutaka kuipindua serikali ya Rais Joseph Kabila
Wendesha mashtaka walisema kuwa washukiwa hao ni wanachama wa kundi la waasi la (Union of Nationalists for Renewal, UNR, nchini DRC.
Polisi wa kupambana na ugaidi waliwakamata washukiwa hao katika mkoa wa kaskazini, Limpopo.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imekumbwa na uasi wakati wote wa utawala wa Kabila.
Aliingia mamlakani mwaka 2001,baada ya mauaji ya babake, Laurent Kabila.
Mafunzo maalum
Mmoja wa washukiwa wa njama ya mapinduzi ametambuliwa kama raia wa Marekani James Kazongo, kulingana na ripoti za shirika la habari la AP
''Washukiwa hao waliingia Afrika Kusini kupanga mafunzo maalum ya kijeshi kwa lengo la kumpindua rais Kabila,'' alisema kiongozi wa mashtaka Shaun Abrahams.
''Walikuwa wameahidi kuwokodisha mamluki ambao wangewalipa kwa kuwapa migodi ya dhababau nchini DRC,'' alisema bwana Abrahams.
Polisi nchini walipokea taarifa kuhusu kuwepo nchini humo kwa washukiwa hao, mwezi Septemba mwaka jana.
Kuna makundi mengi ya waasi wanaoendeshea harakati zao Mashariki mwa DRC.
Eeneo hilo limeathirika kutokana na uasi wa kundi la M23 ambalo limelazimisha takriban watu laki nane kutoroka makwao.

0 comments: