KIMONDO CHALIPUKA URUSI -CHAJERUHI MAELFU.

http://l1.yimg.com/bt/api/res/1.2/8Wsn.L5hUnOOgtDSkVJBnw--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD00NzE7cT04NTt3PTYzMA--/http://media.zenfs.com/en_us/News/Reuters/2013-02-15T101834Z_1461539070_GM1E92F1EHS01_RTRMADP_3_RUSSIA-METEORITE.JPG

MOSCOW URUSI,
Maelfu ya watu wameripotiwa kujeruhiwa na vipande vya nyota aina ya kimondo na vioo vya nyumba pamoja na mipasuko mingine iliyotokana na kulipuka kwa nyota hiyo inayokadiriwa kuwa na uzito wa tani zaidi ya 10.

Mashuhuda wamesema mlipuko huo umetokea huko Moscow na waliona mwanga pamoja na kusikia mlio mkubwa kutoka angani ambao uliangusha vipande na kusababisha madirisha kupasuka vioo.

Watu wengi waliingiwa na hofu kwa kudhani ni mwisho wa dunia au shambulio la Bomu, ingawa walitolewa hofu hiyo na vyombo vya habari.Wataalamu wa mambo ya anga wamesema kitu kama hicho ni cha kawaida katika mizunguko ya sayari na kuwataka watu wasiwe na hofu kuhusu msatakabali wa dunia.

0 comments: