CLINTON AJIUZURU RASMI,ADAIWA KUTAKA KUGOMBEA URAIS 2016
WASHINGTON-MAREKANI,
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hillary Rodham Clinton amejiuzuru rasmi hapo Ijumaa ya jana akimaliza miaka mine ya kulitumikia taifa hilo kama waziri wa ulinzi.Katika barua yake kwa rais Obama waziri huyo amemshukuru rais huyo kwa kumpa nafasi ya kutumikia katika utawala wake akisema nafasi hiyo imempa heshima.
"Ninaamini katika uongozi wa Marekani katika ulimwengu kama nguvu katika kuleta ulimwengu bora" alisema Bi.Clinton.
Kujiuzuru kwa waziri huyo kumeanza baada ya kuapishwa kwa John Kerry jana hiyo.
Licha ya kuwa kujizuru huko ni kwa kawaida Bi,Clinton ameacha lawama kwa uongozi wa rais Obama kutokana na kuonekana kutowajibika kuzuia shambulio la ubalozi wa Marekani hapo Septemba mwaka jana ambapo lilimuua balozi wa Marekani nchini humo.Ingawa kwa upande wake Bi.Clinton amekuwa akishindwa kukubali moja kwa moja kuwajibika huko akisema hakuna ushahidi dhahiri wa kuonesha kushindwa au kuzembea kwake katika tukio hilo.
Katika hatua nyingine kumekuwepo na tetesi za mama huyo kugombea urais hapo mwaka 2016, huku Bi.Clinton akisema kwa sasa anaenda kupumzika na atafikiria kuhusu uamuzi huo ingawa amesema tukio la Benghazi halitoathiri uamuzi wake wa kugombea Urais mwaka 2016.(YAHOO NEWS)
0 comments: