ECOWAS WAHAIRISHA MKUTANO WA MALI.
Imeripotiwa kuwepo kwa maandamano makubwa katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo Bamako na uwanja wa ndege nchini Mali katika eneo la kupaa na kutua hali inayofanya usafiri kuwa mgumu kwa njia ya anga nchini humo.
Siku ya Jumatano maelfu ya wananchi wa Mali waliandamana kupinga kuingiliwa na nchi za kigeni huku wakiyaunga mkono maandamano hayo.
Wakati huo huo nchi jirani na Mali zikiwemo Ivory Coast na ghana zimetishia kufunga mipaka yao inayopakana na nchi hiyo kuanzia saa72 zijazo ikiwa majeshi ya waasi hayatakabidhi madaraka kwa wananchi.Pia nchi zote za ECOWAS zimesema zitaizuia mali kutumia bandari zao katika usafiridhaji. Kikwazo kingine ni kufungwa kwa akaunti ya serikali ya nchi hiyo katika benki ya Ukanda wa magharibi ya ECOWAS pia benki hiyo imezuiwa kutoa pesa kwa benki binafsi nchini Mali.
0 comments: